32 ـ باب: احفظ الله يحفظك

Hadith No.: 85

85 - عَن ابْنِ عَبَّاسٍ قَالَ: كُنْتُ خَلْفَ رَسُولِ اللهِ صلّى الله عليه وسلّم يَوْماً فَقَالَ: (يَا غُلاَمُ، إِنِّي أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ، احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَألْتَ فَاسْأَلِ اللهَ، وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللهِ، وَاعْلَمْ أَنَّ الْأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أَنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إِلاَّ بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وَلَوْ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إِلاَّ بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الْأَقْلاَمُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ) .

Kutoka kwa Abdillah bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Nilikuwa nyuma ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake siku moja Akasema: Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno: "Muhifadhi Mwenyezi Mungu atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta uendako, utakapoomba basi muombe Mwenyezi Mungu, na utakapotaka msaada basi taka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na tambua yakuwa umma lau ungelikusanyika juu ya kukunufaisha wewe wasingelikunufaisha ila kwa kitu alichokiandika Mwenyezi Mungu kuwa kikunufaishe, na kama watakusanyika juu ya kukudhuru wewe kwa kitu chochote, hawatoweza kukudhuru ila kwa kitu alichokiandika Mwenyezi Mungu kuwa kitakudhuru, kalamu zimenyanyuliwa, na kurasa zimekauka". Na katika riwaya nyingine: "Muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, jipendekeze kwa Mwenyezi Mungu wakati wa raha atakujua wakati wa shida, najua kuwa yaliyokukosa hayakuwa ni yenye kukupata, na yaliyokupata hayakuwa ni yenye kukukosa, najua kuwa msaada (nusra) huendana pamoja na subira, nakuwa faraja huendana pamoja na matatizo, na hakika palipo na uzito pana wepesi".

قال تعالى: {وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنْتُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ}. [الحديد:4]

[ت2516]

85 - زاد في رواية لأحمد: (تَعَرَّفْ إِلَيْهِ فِي الرَّخَاءِ يَعْرِفْكَ فِي الشِّدَّةِ... وَاعْلَمْ أَنَّ فِي الصَّبْرِ عَلَى مَا تَكْرَهُ خَيْراً كَثِيراً، وَأَنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْراً) .

قال تعالى: {وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنْتُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ}. [الحديد:4]

[حم2801]

* صحيح.