الكتاب الأول: الطعام والشراب

قال تعالى: {يَاأَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ *}. [البقرة:172] وقال تعالى: {يَاأَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا *}. [المؤمنون:51]

2638 - (ق) عَنْ عُمَرَ بْنِ أَبِي سَلَمَة قَالَ: كُنْتُ غُلاَماً في حَجْرِ [1] رَسُولِ اللهِ صلّى الله عليه وسلّم، وَكانَتْ يَدِي تَطِيشُ [2] في الصَّحْفَةِ، فَقَالَ لِي رَسُولُ اللهِ صلّى الله عليه وسلّم: (يَا غُلامُ، سَمِّ الله، وَكُلْ بِيَمِيِنكَ، وَكُلْ مِمَّا يَلَيكَ) ، فَمَا زَالَتْ تِلْكَ طِعْمَتِي [3] بَعْدُ.

Kutoka kwa Omar bin Abii Salama Amesema: Nilikuwa kijana katika malezi ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, na ulikuwa mkono wangu ukizunguka pande zote katika sahani (ya chakula) Akasema kuniambia mimi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Ewe kijana, mtaje Mwenyezi Mungu, na ule kwa mkono wako wa kulia, na ule chakula kilichopo mbele yako" kinachokuelekea" Basi sikuacha tena kula kama nilivyoelekezwa baada ya hapo.