Kutoka kwa Abuu Saidi na Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, ispokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake".
Kutoka kwa Abuu Musa Al Ash'ariy radhi za Mwenyezi ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Atakapougua mja au akasafiri ataandikiwa malipo sawa na mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa mkazi na mzima wa afya".