Kutoka kwa Ma'qili bin Yasari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakuna mja yeyote atakayempa Mwenyezi Mungu raia, akafa siku anakufa, haliyakuwa aliwafanyia ghushi (udanganyifu) ispokuwa atamharamishia Mwenyezi Mungu pepo".
Kutoka kwa bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakika ukweli ni kwamba utakuja kutokea uchoyo baada yangu na mambo msiyoyajua(uzushi)!" wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki iliyo juu yenu, na mumuombe Mwenyezi Mungu haki yenu".
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema: "Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga, na atakayepigana chini ya bendera kibubusa anachukia kwasababu ya ndugu zake, au akahamasisha katika (kupendelea kwasababu ya) udugu, au ana nusuru udugu, akauwawa, basi hicho ni kifo cha zama za ujinga, na atakayejitoa katika umma wangu, akimpiga mwema wake na muovu wake, na wala hajali muumini wake, na wala hamtimizii mwenye ahadi ahadi yake, basi huyo si miongoni mwangu na mimi si miongoni mwake".