Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia".
Kutoka kwa Suhaibu bin Sinani Al Ruumiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini: akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake".
Kutoka kwa Mustaurid bin Shaddadi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Si chochote dunia katika Akhera isipokuwa ni kama mfano wa mmoja wenu anapoweka kidole chake baharini, kisha atazame kimerudi na nini!"