Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakika muumini hufikia kwa tabia yake njema nafasi ya mfungaji mwenye kusimama usiku".
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze, Na Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu jirani yake, Na Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu mgeni wake".
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake Amesema: "Haijawahi kupunguza sadaka chochote katika mali, Na hajawahi kumzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa usamehevu (wake) ispokuwa utukufu, na hajawahi kunyenyekea yeyote ispokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimnyanyua".