Kutoka kwa Muawiya bin Abii Sufiyani- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie: "Mwenye kumtakia Mwenyezi Mungu kheri kwake humpa ufahamu katika dini".
Kutoka kwa Abdillahi bin Amri bin Aaswi- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao-: Yakwamba Mtume Rehema na Amani zimfikie Amesema: "Fikisheni toka kwangu walau Aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna tabu, na atakayenizulia uongo juu yangu kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake motoni".