Kutoka kwa Abuu Qatada Al-Answariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea".
Kutoka kwa Ally bin Abii Twalib -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: (Nilikuwa ni mtu mwenye madhii mengi, nikaona haya kumuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwasababu ya nafasi ya binti yake kwangu, nikamtuma Mikidadi bin Aswadi akamuuliza, akasema: Ataosha tupu yake, na atatawadha) Na kwa Bukhariy: (Osha tupu yako na utawadhe). Na kwa Muslim: (Tawadha na usafishe tupu yako).
Kutoka kwa Abuu Ayyub Al-answariy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi". Akasema Abuu Ayyub: "Tukaenda sham, tukakuta vyoo vimejengwa kuelekea upande wa kibla, tukawa tunapinda, na tunamuomba Mwenyezi Mungu msamaha".