Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Nimepewa mambo matano, hajapewa yeyote katika manabii kabla yangu: nimenusuriwa (nimeepushwa) na hofu kiasi cha kutembea mwezi mzima, na imefanywa ardhi kwangu kuwa ni msikiti na ni mahala twahara (safi), Hivyo basi mtu yeyote katika umma wangu itakapomkuta swala basi na aswali, na nimehalalishiwa kwangu ngawira, na hazikuhalalishwa kwa yeyote kabla yangu, na nimepewa utetezi, na alikuwa Nabii yeyote anatumwa kwa watu wake tu, na mimi nimetumwa kwa watu wote"
Kutoka kwa Abdallah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiitembelea msikiti wa Qubaa kwa kipando na kwa miguu, anaswali ndani yake rakaa mbili. Na katika riwaya nyingine: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akienda msikiti wa Qubaa kila juma mosi akiwa katika kipando na kwa miguu, na alikuwa bin Omar akifanya hivyo.