Kutoka kwa Abi Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: amesema Mtume Muhammad Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake: ((Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?)) wakasema: ndiyo, Ewe Mtume wa Allah, akasema: ((Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri)).
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, Amesema: "Swala tano, na Ijumaa mpaka Ijumaa, na ramadhani mpaka ramadhani vinafuta madhambi yaliyo kati yake, yatakapoepukwa madhambi makubwa".