Kutoka kwa Abdillahi bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Nilisali pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- rakaa mbili kabla ya adhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Ijumaa, na rakaa mbili baada ya magharibi, na rakaa mbili baada ya ishaa" Na katika lafudhi nyingine: "Na ama magharibi na ishaa na ijumaa: hizo aliswalia nyumbani". Na katika tamko lingine: Nikuwa Bin Omar alisema: Alinisimulia Hafswa: kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Alikuwa akisali sijida mbili nyepesi (fupi) baada ya kuchomoza alfajiri, na zilikuwa ni nyakati ambazo siingii kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-".