Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Amesema Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka-: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yakwangu na mimi ndiye ninayeilipa, na funga ni kinga, itakapokuwa ni siku ya kufunga mmoja wenu, basi asifanye mambo machafu, na wala asifanye vurugu, ikiwa mtu atamtukana au kumpiga basi na aseme: Hakika mimi nimefunga, Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake hakika harufu ya kinywa cha mtu aliyefunga ni nzuri zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko hata harufu ya miski, mfungaji ana furaha mbili anazozifurahia: Anapofuturu hufurahia kufuturu kwake, na atakapokutana na Mola wake atafurahia swaumu yake". Na hili ni tamko la riwaya ya Bukhariy. Na riwaya nyingine ya kwake: "Anaacha chakula chake na kinywaji chake, na matamanio yake kwaajili yangu, swaumu ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa, na jema moja ni sawa na mema kumi mfano wake". Na katika riwaya ya Muslim: "kila amali ya mwanadamu hulipwa mara dufu, jema moja ni sawa na mema kumi mfano wake mpaka inafika zaidi ya mia saba, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Isipokuwa swaumu hakika hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa; anaacha matamanio yake na chakula chake kwaajili yangu, mfungaji anafuraha mbili: furaha wakati kufuturu kwake, na furaha wakati wa kukutana kwake na Mola wake, na harufu mbaya ya kinywa chake ni nzuri sana mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko hata harufu ya miski".
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Hadithi Marfu'u: "Atakayefunga ramadhani kwa imani na kwa kutaraji malipo, atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake".