Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Umma wangu wote utaingia peponi ispokua atakaye kataa, akaulizwa ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani atakaye kataa? akajibu: Mwenye kunitii ataingia peponi na mwenye kuniasi atakuwa amekataa".
Kutoka kwa Abdillah bin Masudi-Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehma na amani ziwe juu yake- " Amesema: Wameangamia wenye kujilazimisha -Alilisema hilo mara tatu-"