Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie Amesema: "Swala nzito juu ya wanafiki: ni swala ya ishaa na swala ya Alfajiri, na lau wangejua yaliyomo ndani ya swala hizo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilitamani niamrishe swala ikimiwe, kisha nimuamrishe mtu awaswalishe watu, kisha niondoke wakiwa pamoja nami wanaume wakiwa na vijinga vya moto twende kwa watu ambao hawahudhurii swala nikazichome nyumba zao kwa moto".
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudriy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie: "Mtakapomsikia muadhini basi semeni mfano wa jinsi anavyosema".