17 ـ باب: الإيمان والإسلام والإحسان

Hadith No.: 49

49 - (م) عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صلّى الله عليه وسلّم ذَاتَ يَوْمٍ، إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَيَاضِ الثِّيَابِ، شَدِيدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لاَ يُرَى عَلَيْهِ أَثَرُ السَّفَرِ، وَلاَ يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ صلّى الله عليه وسلّم، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَوَضَعَ كَفَّيْهِ عَلَى فَخِذَيْهِ [1] ، وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ، أَخْبِرْنِي عَنِ الإِسْلاَمِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صلّى الله عليه وسلّم: (الإِسْلامُ: أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لاَ إِلهَ إِلاَّ اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللهِ صلّى الله عليه وسلّم، وَتُقِيمَ الصَّلاَةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصُومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ البَيْتَ، إِنِ اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبِيلاً) ، قَالَ: صَدَقْتَ.قَالَ: فَعَجِبْنَا لَهُ، يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقُهُ [2] . قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الإِيمَانِ؟ قَالَ: (أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلاَئِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ، وَاليَوْمِ الآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ) ، قَالَ: صَدَقْتَ.
قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الإِحْسَانِ؟ قَالَ: (أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ، فَإِنَّهُ يَرَاكَ) .
قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ السَّاعَةِ؟ قَالَ: (مَا المَسْؤُولُ عَنْهَا بِأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ) . قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنْ أَمَارَتِهَا
[3]
؟ قَالَ: (أَنْ تَلِدَ الأَمَةُ رَبَّتَهَا، وَأَنْ تَرَى الحُفَاةَ العُرَاةَ، العَالَةَ [4] ، رِعَاءَ الشَّاءِ، يَتَطَاوَلُونَ فِي البُنْيَانِ) .
قَالَ: ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيّاً
[5]
، ثُمَّ قَالَ لِي: (يَا عُمَرُ! أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ) ؟ قُلْتُ: اللهُ ورَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: (فَإِنَّهُ جِبْرِيلُ، أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ) .

Kutoka kwa Omar Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: "Tukiwa sisi tumekaa kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- siku moja, ghafla akatokeza mwanaume mmoja, mwenye nguo nyeupe sana, mwenye nywele nyeusi sana, hazionekani kwake athari za safari, na wala hakuna anayemfahamu yeyote katika sisi, mpaka akakaa kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akashijanisha magoti yake katika magoti mtume Rehema na Amani ziwe juu yake (mfano wa kikao cha tahiyatu) na akaweka mikono yake juu ya mapaja yake, Na akasema: Ewe Muhammadi, nieleze kuhusu Uislamu? Akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: Uislamu ni kushuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na usimamishe swala na utoe zaka, na ufunge Ramadhani, na uhiji nyumba tukufu ukipata uwezo wa kuifikia, Yule bwana akasema: "Swadakta"-Yaani: Umesema kweli, Tukamshangaa! Anamuuliza na anamsadikisha! Akasema: Nieleze kuhusu Imani? Akasema: Ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho, na uamini makadirio kheri yake na shari yake, Akasema: "Swadakta"-Yaani: Umesema kweli, Basi hebu nieleze kuhusu Ihsani (wema)? Akasema: Ni umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba wewe unamuona, na ikiwa wewe humuoni basi yeye anakuona: Akasema: Hebu nieleze kuhusu kiyama: Akasema: hakuwa muulizwaji kuhusu hilo ni mjuzi kuliko muulizaji, Akasema: Hebu nieleze kuhusu dalili zake? Akasema: ni mjakazi kuzaa bwana yake, na ukawaona watembea peku na uchi na masikini wachunga mifugo wakishindana kujenga majengo marefu, kisha yule bwana akaondoka, akakaa muda kidogo kisha akasema: Ewe Omari unamjua ni nani huyo muulizaji? Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, Akasema: Basi bila shaka huyo ni Jibril alikuijieni ili akufundisheni dini yenu".

قال تعالى: {إِنَّ الدِّينَ عِنْدَ اللَّهِ الإِسْلاَمُ}. [آل عمران:19] وقال تعالى: {وَمَنْ يَكْفُرْ بِاللَّهِ وَمَلاَئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلاَلاً بَعِيدًا}. [النساء:136] وقال تعالى: {وَأَحْسِنُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ}. [البقرة:195]

[م8]