23 ـ باب: الذكر بعد الصلاة

Hadith No.: 1253

1253 - (م) عَنْ ثَوْبَانَ قَالَ: كَانَ رَسُولُ الله صلّى الله عليه وسلّم، إِذَا انْصَرَفَ مِنْ صَلاَتِهِ، اسْتَغْفَرَ ثَلاَثاً، وَقَالَ: (اللَّهُمَّ! أَنْتَ السَّلاَمُ وَمِنْكَ السَّلاَمُ، تَبَارَكْتَ ذَا الجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ) .

Kutoka kwa Thauban -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehma na Amani ziwe juu yake- anapomaliza swala yake anataka msamaha mara tatu, na anasema: Allaahumma antas salaam, waminkas salaam, Tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam (Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe ni Amani, na Amani hutoka kwako, umetakasika Ewe mwenye Utukufu na ukarimu).

[م591]