Kutoka kwa Abii Bakra Nufa'i bin Harith Ath thaqafiy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake Amesema: "Watakapo kutana waislamu wawili kwa mapanga yao basi muuwaji na muuliwaji wote motoni" Nikasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, huyu muuwaji sawa, na vipi huyu muuliwaji? Akasema: "Hata yeye alikuwa na pupa ya kumuuwa mwenzie".
Kutoka kwa Abdallah bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-Hadithi Marfu'u: "Haitokei kuuliwa nafsi yoyote kwa dhulma isipokuwa hupata binadamu wa mwanzo fungu (la dhambi) kutoka katika damu hiyo, kwasababu yeye ndiye muanzilishi wa kwanza kuua".
Kutoka kwa Abdallah bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- : "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".